Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Related image
Mchana wa September 7 2017 zilienea taarifa za mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Area D Dodoma ndani ya gari yake akiwa katokea Bungeni.
Tundu Lissu baada ya tukio hilo alikimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma na kupatiwa wa matibabu, watu wengi wameguswa kuhusiana na tukio hilo wakiwemo wanasoka wa Tanzania na nahodha wa timu ya taifa y Tanzania anayechezea club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta.
Mastaa wa soka kama Juma Abdul wa Yanga, Deus Kaseke wa Singida United, golikipa wa Taifa Stars na Simba Sports Aishi Manula, golikipa wa zamani wa Simba anayeichezea Singida United kwa sasa Peter Manyika Junior na Mbwana Samatta wametumia kurasa zao za instagram kuoneshwa kuguswa na tukio hilo.
Post ya Samatta “Hii sio habari nzuri Mungu atamponya tumuombee, so sad”
Samatta
Deus Kaseke “Play For Tundu Lissu”
Deus Kaseke
Post ya Juma Abdul “Kwa uwezo wa Allah tuseme inshaallah”
Kwenye picha katikati ni Juma Abdul
Post ya Aishi Manula
Aishi Manula
Post ya Peter Manyika Junior

Post a Comment

 
Top