Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Moja kati ya stori ambazo zimewashitua wengi Ijumaa ya leo September 1 2017 ni kuhusiana na maamuzi ya Mahakama Kuu nchini Kenya kubatilisha matokeo ya uchaguzi Mkuu uliyofanyika August 8 2017 na Uhuru Kenyata kuibuka mshindi wa Urais dhidi ya Raila Odinga.
Jaji Mkuu David Maraga ameagiza uchaguzi Mkuu mpya utafanyika ndani ya siku 60 kwa mujibu wa sheria na katiba na umebatilishwa kwa sababu IEBC hawakuwa wameandaa uchaguzi huru na haki.
Kila mmoja amepokea uamuzi huo kitofauti, mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ameandika mtazamo wake kupitia ukurasa wake wa instagram “Niliwahi Sema najifunza jambo toka Kenya, Leo inathibitika wakati Mahakama inafungua kurasa Mpya ya Kumbukumbu ya Maamuzi.#KenyaDecides“

Post a Comment

 
Top