Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Moja kati ya ‘couple’ ambayo ilipendwa sana na mashabiki, ni ya wanamuziki, Juma Jux na Vannesa Mdee, ambao kwa sasa wameshapigana kibuti, lakini Jux anaonekana bado anampenda, na anatamani kurudiana na Vannesa, kama alivyoweka wazi katika ukurasa wake wa Instagram, siku ya ‘bethidei yake’.
Jux ambaye leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, aliandika ujumbe unaonyesha wazi, ni kiasi gani anamkumbuka X- wake huyo, hususan inapofika siku yake ya kuzaliwa:Nakumbuka mara ya mwisho kufanya pati ya bethidei yangu ilikuwa 2013, miaka minne iliyopita.Sikuwahi kufanya pati yoyote tena sababu nilikuwa na rafiki, mpenzi na mtu wa karibu kuliko mtu yeyote kwenye maisha yangu. Miaka yote iliyofata nilikuwa na yeye mpaka sasa hatuko tena karibu kama mwanzo.
“Tumebaki kuwa marafiki wa kawaida tu uwepo wake tu ulikuwa ni zaidi ya chochote kwenye siku yangu ya kuzaliwa, kuongea na yeye au text yake tu ilitosha kukamilisha siku yangu.
“Ila sasa sidhani kama itakuwa kama mwanzo nitafarijika sana kama nitamuona leo.”

NA ISRI MOHAMED/GPL

Post a Comment

 
Top