Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MSANII wa muziki wa RNB nchini, Juma Jux, anayetamba na wimbo wake mpya wa ‘Utaniua’ amefunguka juu ya uhusiano wake na mwanamuziki wa Tanzania, Vanessa Mdee, kuwa kwake kwanza ni familia yake halafu anafuata Vanessa Mdee.
Alipoulizwa na mtandao huu kuhusu uhusiano wake na Vanessa, alisema: ”Nampenda Vanessa kuliko msichana yeyote yule na sitegemei kumuacha, hata familia yangu inajua kuwa nina upendo Mkubwa kwa Vanessa.
“Nikiwaga mbali na Vanessa huwaga asubuhi nikiamka cha kwanza naingiaga Instagram kumuangalia baada ya hapo ndo nampigia simu siwezi, kumpigia simu bila kuangalia picha zake. Kiufupi nampenda sana Vanessa,“ alisema Jux.
Kuhusu kupata mtoto, Jux alifunguka kwamba: “Sa’hivi natamani kupata mtoto na nina mpango huo kwa sasa wa kujipanga kupata mtoto na mpenzi wangu pia mtoto wangu wa kwanza nataka nimuite jina la Karim na si jina jingine zaidi ya hilo.”

NA SAMSON JEREMIAH/GPL

Post a Comment

 
Top