Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Baada ya siku chache kupita toka dirisha la usajili kwa vilabu vya soka barani ulaya lifungwe, kocha wa Man United Jose Mourinho amekuwa muwazi na kueleza kuwa hakuridhia maamuzi ya kuondoka kwa Andreas Pireira na kujiunga na Valencia ya Hispania kwa mkopo.
Andreas Pereira mwenye umri wa miaka 21 ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, ameondoka Man United na kujiunga na Valencia ya Hispania kwa mkopo, maamuzi ambayo kocha wa Man United amethibitisha kutoridhishwa nayo.

Mourinho akizungumza hayo kuelekea game ya Man United dhidi ya Stoke City ya Ligi Kuu England amesema” kuondoka kwa Andreas huo ulikuwa ni uamuzi binafsi ambao mimi sikukubaliana nao kiukweli”>>>Mourinho

Andreas baada ya kutua Valencia
Pereira ambaye alikuwa sehemu ya wachezaji wa Man United waliyosafiri na timu katika maandalizi ya msimu mpya wa Ligi, hakupata nafasi ya kuanza katika mechi tatu za mwanzo za EPL za Man United, hivyo akaamua kwenda Valencia kwa mkopo ambao una kipengele cha kurudi Man United muda wowote Mourinhoatakaomuhitaji.

Post a Comment

 
Top