Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide.
STAA mkongwe kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide amemaliza mkataba wake na Lebo ya Rockstar4000 ambayo pia husimamia kazi za msanii Ali Kiba.
Hivi karibuni Jaydee ambaye kwa sasa ameanza kukiki tena kwenye spika za ‘wana’ kupitia songi lake la I Miss You ambalo yeye amechana na kuimba, alisikika akikiri kumaliza project yake na Rockstar4000 iliyosimamia shoo ya Naamka Tena na sasa yupo mwenyewe.
…Akifanya yake.
“Kwa sasa sipo Rockstar, nimemaliza ile project (Naamka Tena Concert) na Seven (Mosha) kwa hiyo kwa sasa sipo kule,” alisikika Jaydee.
Championi Jumamosi halikulaza damu kwani lilimvutia waya Seven ambaye ni meneja wa lebo hiyo na akakiri kuwa Jide amemaliza mkataba: “Ni kweli kuwa Jide tumemalizana kwani tulikuwa na mkataba naye wa mwaka mmoja na sasa umeisha hivyo hayupo kwenye Lebo ya Rockstar4000

Post a Comment

 
Top