Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Rais wa Mahakama Kuu ya Kenya (Supreme Court), Jaji David Maraga anasemekana kukataa kiasi cha Kshs. 500,000,000 zilizowekwa kwenye akaunti yake ya benki ya KCB Alhamisi mchana.
Kwa mujibu wa Makao makuu ya KCB yaliyopo KENCOM house Nairobi, akaunti ya Dr. Maraga ilipokea pesa hizo saa tisa mchana kutoka kwa mtu asiyejulikana ambaye kwa mujibu wa Jaji huyo ana lengo la kumchafua yeye na mahakama.
Meneja wa tawi wa KCB, Bw. Kamau Ndung’u amesema Bwana Maraga ametaka pesa hizo zirudishwe zilipotoka kwani hakutegemea pesa kutoka kokote na wao kama benki watafanya hivyo mara moja na pia watajitahidi kumpata mtu aliyeweka pesa hizo ili kuweka mambo sawa na wazi.

Post a Comment

 
Top