Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, akihutubia waumini wa kiislamu.
Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuberi akisoma ujumbe wa Eid El Hajj kwa Watanzania.
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh, Alhad Mussa, akizungumza katika sherehe hizo.
Baadhi ya Waislam waliofika kwenye sherehe hizo.
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dk Hussein Mwinyi, leo amewaongoza waumini wa Kiislamu katika kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj ambayo ni maarufu kama ‘Eid ya Kuchinja’.Mwinyi amesisitiza suala la amani kwa Watanzania wote huku akikazia maneno ya Mufti Zuberi aliyokuwa ameyatamka ili waumini waweze kubadilika, akimaanisha kuondokana na dhana zote potofu zisizokuwa na manufaa katika kulijenga taifa chini ya Rais Magufuli na serikali yake.Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Masjid Taqwa, Ilala-Bungoni jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 1:30 asubuhi ambapo Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa na Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuberi, na viongozi wengine wamehudhuria sherehe hizo.Akizungumza katika viwanja hivyo, Zuberi amesema kuwa anawatakia Waislamu kote nchini na wananchi kwa jumla sikukuu njema ya Eid El Hajj ili kila mmoja aisherehekee kwa utulivu na mshikamano.Amewataka pia walimu kote nchini wa shule za Kiislamu za madrasa kufanya jitihada kubwa ya kuhakikisha wanawaelimisha wanafunzi wao ili waweze kuwa na maadili mema na si kuwapatia elimu ya dini yao tu, bali wafundishwe pia masomo mbalimbali ili kuwawezesha kuwa na maadili mema na utaalam unaotakiwa katika maisha yao ya baadaye na kuwa viongozi bora.

Mufti alitoa miezi sita kwa taasisi iliyokuwa na jukumu la kuwasafirisha mahujaji kwenda Makka na kushindwa kufanya hivyo, irudishe fedha ilizokuwa imezichangisha kutoka kwa waumini waliotegemea kwenda huko.

Alisema waumini hao wataweza kwenda kuhiji huko Makka mwaka kesho na kwamba uongozi wake utahakikisha tatizo kama hilo haliwezi tena kujitokeza na kuathiri safari za mahujaji.

NA DENIS MTIMA/GPL

Post a Comment

 
Top