Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Wakati Watanzania wakiendelea kujiuliza kuhusiana na nani ni baba wa mtoto wa Mwanamitindo machachariBongo, Hamisa Mobetto, amezua tena utata kufuatia picha zinazosambaa mitandaoni zikimuonyesha akiwa katika mavazi mithili ya bibi harusi.Baada ya picha hizo kutapakaa kila kona, utata ukawa ni, je Hamisa kafunga ndoa? Na kama ni ndoa kaolewa na nani? ni yule yule msanii wa Bongo Fleva au?
Baadhi ya mashabiki wakasema kwamba kama ni ndoa na ameolewa na yule mwanamuziki anayehisiwa kuzaa naye, basi anapendwa sana maana anavyoonekana na alivyopendeza kama siyo mchepuko vile.
Kauli ya ‘kama siyo mchepuko vile’, ni kwa sababu mwanamuziki huyo ni mzazi mwenza na Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’, hivyo kitendo cha Mobetto kuzaa na kufunga naye ndoa, huku akivimba na picha zake kwenye mitandao ya kijamii, basi atakuwa anajiamini kama mmiliki halali wa Mbongo Fleva huyo.
Hata hivyo haijafahamika kama picha hizo ni za harusi ya kweli au ni ‘project’.

NA ISRI MOHAMED/GPL

Post a Comment

 
Top