Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mtandao wa express.co.uk umeripoti taarifa ambazo haziwezi kuwa nzuri kwa shabiki wa FC Barcelonakuhusiana na kiungo wao wa kimataifa wa Hispania Andre Iniesta, staa huyo ameripotiwa kuwa mbioni kuihama club hiyo mwisho wa msimu licha ya kupewa ofa mpya.
Iniesta mwenye umri wa miaka 33 mkataba wake na FC Barcelona unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2017/18 lakini ameonesha dalili zote za kutotaka kuongeza licha ya Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeuamenukuliwa na Mundo Deportivo kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba na staa huyo.
“Tayari tumeshafikia makubaliano ya mwanzo ya kumuongezea mkataba mpya, natumaini tutakamilisha katika wiki zijazo lakini bado tunaendelea kuzungumza nae kwa sababu ni mchezaji ambaye tungependa kuona akistaafu akiwa hapa atakapojisikia kufanya hivyo” >>>Josep Maria Bartomeu

Josep Maria Bartomeu

Hata hivyo Iniesta amenukuliwa na gazeti la AS baada ya kuulizwa umefikia makubaliano yoyote na Barcelonakuongeza mkataba mpya? jibu lake lilikuwa “Hapana”

Post a Comment

 
Top