Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg na mkewe Priscilla Chan ndio watu pekee ambao huwezi kuwablock katika mtandao maarufu wa kijamii wa Facebook.
Mark Zuckerberg na mke wake
Mwanzoni kabla ya Mark Zuckerberg kumuoa Priscilla ni yeye pekee ndiye ambaye hakukuwa na uwezekano wa Kumbloku. Mark huandika taarifa nyingi kuhusu maboresho ya Facebook na taarifa mbalimbali kuhusu maisha yake binafsi au mambo mengine ya kijamii.
Kublock mtu ni njia mojawapo ya kutotaka mtu aone posti zako wala zake. Njia hii unaweza kufanya asiwe rafiki yako (Unfriend) au kukufuata (Unfollow)
Muanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg abadili mtazamo wake juu ya dini Mark Zuckerberg na Priscilla Chan walikutana mwaka 2003 wote wawili wakiwa wanafunzi chuo kikuu cha Havard, na mwaka 2012 walioana baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu.
Kwa mujibu wa ripoti ndani ya The Independent, machapisho yote (ndani ya facebook) huonekana katika mifumo ya malekezo ya kitarakimu ya Facebook inayofahamika kama ‘algorithm’ na mwishowe kuzipeleka kwa wachangiaji mbalimbali.
Hivyo kumzuia mwasisi wa Facebook na mkewe kulikuwa ndiyo njia mwafaka ya kuepuka machapisho yanayorushwa kwenye kurasa za mtandao huo kuonekana kabla ya kupigwa kabisa marufuku. Zuio (Block) hilo limekuwapo tangu mwaka 2010

Post a Comment

 
Top