Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwanaisha Nyange ‘Dayna Nyange’.
MWANADADA ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Chovya, Mwanaisha Nyange ‘Dayna Nyange’, hivi karibuni amemtolea povu mkali aliyewahi kutamba na Wimbo wa Dua la Kuku, Nas B kuwa asitafute kiki kupitie yeye.Akichonga na Showbiz, Dayna alisema kuwa amekuwa akisikia kutoka kwa watu wake wa karibu na kuona mitandaoni kwamba Nas B ambaye pia ni Prodyuza wa Pamoja Records, anadai kumpenda lakini hajapata nafasi tu ya kumfi kia.
Huwezi kumpenda mtu na kuonesha hisia zako kupitia mitandaoni, kama yeye ananipenda kwa nini asinitafute na tuzungumze mpaka aandike mitandaoni kwamba ananitafuta bila mafanikio, huyo msanii asitafute kiki kupitia mimi!” alisema Dayna Nyange.
Baada ya Dayna kutokwa povu Showbiz iliamua kumtafuta Nas B ambaye alifunguka kuwa;
“Ni kweli ninampenda Dayna lakini sijapata nafasi ya kuonana naye.
Nimewahi kumpigia simu lakini hakupokea ndiyo maana nikaona niweke wazi kupitia mtandao wa Instagram, lakini kama hajapenda anisamehe na nitamtafuta niweze kumweleza hisia zangu nikiwa naye ana kwa ana.”

Post a Comment

 
Top