Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Usiku wa August 27 2017 Bondia mwenye sifa ya kutopoteza pambano hata moja Floyd Mayweather alirudi ulingoni kucheza pambano la 50 dhidi ya Mc Gregor hiyo ikiwa ni muda umepita toka apigane na Manny Pacquiao na kumpiga.
Mc Gregor ambaye alionekana kuwa na tambo alipigwa na Mayweather kwa Technical Knock Out (TKO)round ya 10 pambano la round 12, huo ukawa ni mwisho wa tambo zake dhidi ya Mayweather, licha ya kipigo hicho Mc Gregor kupanda tu ulingoni kulimfanya aingize dola milioni 100 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 200 za kitanzania.
Leo September 10 2017 Mc Gregor anayetokea Ireland ameonekana akiwa amekodi boti binafsi akiwa na familia yake wanaendelea kula bata Hispania katika fukwe za Ibiza, kitu ambacho wengi wanaamini anatumia au ana furaha kuingiza Dola milioni 100 licha ya kupoteza.Mc Gregor na Mayweather walipopambana

Post a Comment

 
Top