Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Waswahili wanasema “Umri ni namba” wakikusudia unaweza kuwa na miaka mingi lakini wajihi wako ukakutambulisha kama mwenye umri wa kati na wapo watu mbalimbali hasa maarufu ambao mara zote unazoweza kumuona huwa katika muonekano ule ule licha ya umri wake kusogea.
Sasa leo September 2, 2017 ninayo list ya mastaa sita ambao wana umri mkubwa lakini muonekano wao hauoneshi kama umri umeenda.

1. Pharrell Williams

Ni mwimbaji wa miondoko ya Pop, mwandishi wa nyimbo na producer. Ana umri wa miaka 44 lakini anaonekana tofauti kabisa na ulivyo umri wake. Picha hii ina tofauti ya miaka 11.

2. Gwen Stefani

Ifikapo October 3 Mwanamuziki Gwen atakuwa anatimiza umri wa miaka 48, ana mume na watoto watatu. Katika picha hii hapa chini ni tofauti ya miaka 12.


3. Sandra Bullock

Ni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu wa Marekani ambaye ana umri wa miaka 53. Ana mume na watoto wawili lakini katika picha hii ni tofauti ya miaka 13.


4. Jennifer Lopez

Mwimbaji, muigizaji, mwanamitindo ambaye amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mastaa kibao akiwemo P Did. Ana umri wa miaka 48 na katika picha hii ni tofauti ya miaka 14.


5. Julia Roberts

Inga wa picha hizi zina tofauti ya miaka 20 lakini mwigizaji Julia Roberts ambaye October 28 atatimiza miaka 50 lakini haonekani kuzeeka na bado anaendelea kuwa mrembo kila siku.


6. Will Smith

Mwanamuziki na Mwigizaji ambaye amekuwa na mafanikio zaidi kwenye uigizaji kuliko muziki. Baadaye mwezi huu, September 25 atakuwa na umri wake ni miaka 49 lakini haonekani kufanana na umri huo. Picha hii ina tofauti ya miaka 21

Post a Comment

 
Top