Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


JESHI la Polisi Septemba 12, Kivule chanika lilifanikiwa kumuua jambazi sugu aitwae Anae Rashid kapela aliyekuwa akitafutwa na jeshi hilo kwa muda mrefu akituhumiwa kushiriki matukio mbalimbali ya ujambazi likiwemo la mauaji ya polisi wanane wilayani Kibiti.Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Mambosasa alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar.
“Baada ya kupewa taarifa na wasamalia wema, Jeshi hilo lilifika na kuizingira nyumba alimokuwa lakini alifanikiwa kutoka na kutaka akitoroka. Polisi walipomsimamisha alikimbia ndipo wakampiga risasi ya goti na kuanguka.
“Alipohojiwa aliwataja wenzake pamoja na matukio makubwa ya uhalifu aliyoshiriki kuyafanya likiwemo hilo la kuwaua Askari Polisi wanane na kupora silaha zao kisha kukimbia,” alisema Mambosasa.

Post a Comment

 
Top