Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wanachama wa Uzalendo Kwanza.
KAMPENI ya Uzalendo Kwanza iliyoanzishwa na Wasanii wa Filamu, Bongo Movie imezidi kuota mizizi baada ya kutanua matawi yake kwa mikoa yote ya Tanzania huku ikipata wanachama ambao ni wachezaji wa soka, wasanii wa muziki, wanasiasa na raia wa kawaida hapa nchini.
Wasanii hao wakifuatilia tukio hilo.
Akizungumza na wanahabari wakayi akiwapokea wanachama wapya, Mwenyekiti wa Chama hicho, Steve Mengele ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa lengo la Chama hicho ni kuwafikia Watanzania wote kufahamu umhimu wa uzalendo, kuipenda nchi ikiwa ni pamoja na kushirikiana kikamilifu na serikali ya Rais John Magufuli katika kutimiza majukumu yake.
Wasanii hao wakifuatilia tukio hilo.
“Taifa la wazalendo linaanzia darasani, tunawaomba walimu wote wawe wazalendo kufundisha darasani, manesi na madakatari wawe wazalendo kutoa huduma zao, uzalendo pia ni mhimu kusapoti vilabu vyetu vya soka na Timu ya Taifa,” alisema Nyerere.
Wasanii hao wakifuatilia tukio hilo, kulia ni Duma na Tausi.
Aidha Nyerere amewaasa wanachama hao na Watanzania wote kuunganisha nguvu ya pamoja ili kulinda kazi zao za sanaa sambamba na kuwafanya Watanzania kupenda vilvivyo vyao mfano; kazi za wasanii wa ndani ili kukuza kipato chao na kuinua uchumi wa nchi.
Steve Nyerere akiwatambulisha wanachama wapya ambao ni wachezaji wa zamani wa Soka nchini.
Wacheza soka ambao wamejiunga na Uzalendo Kwanza ni; Mwanamtwa, Monja Liseki, Abdallah Kaburu, Dotto Mokili, Steven Nemes na wengine.
Steve Nyerere akiwatambulisha wanachama wapya ambao ni wasanii wa Bongo Movie.
Mbali na hao, msanii wa Bongo Fleva, Ruby pia amejiunga na Uzalendo Kwanz ambaye amepewa jukumu la kutunga nyimbo za Uzalendo na video zake ili kufikisha ujumbe kwa wananchi wote.


Post a Comment

 
Top