Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Usiku wa September 16 2017 baba mzazi wa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta alifanya interview na kipindi cha Nipe Tanocha TBC 1 na kuzungumza mbalimbali.
Baba yake mzazi na Mbwana Samatta anajulikana kwa jina la Ally Samatta Pazi na amezungumzia vitu mbalimbali kuhusu soka na maisha ya mtoto wake alipotokea Mbwana Samatta, baadhi ya vitu avyozungumza ni kuhusiana na suala la kuoa kwa mwanae.
“Nimemwambia hakuna kuoa hadi atimize miaka 30 sasa hivi ana miaka 25, kwa mfano juzi aliniuliza baba mimi nikioa mzungu vipi? nikasema marufuku kuleta mzungu hapa pamoja na kwamba tutapata faida ya aina fulani fulani lakini marufuku kuleta mzungu Baba Samatta
Kutoka kushoto ni Ally Samatta Pazi ambaye ni baba mzazi wa Mbwana Samatta.
“Sitaki mzungu kwa sababu watamtenga familia kwa sababu watu wanataka wawe huru na mkeo kwa sababu ya lugha sasa namwambia utakosana na ndugu zako lakini kama ikitokea basi imetokea lakini namwambia kama umeoa mzungu basi oa na muafrika”Baba Samatta
“Samatta ana watoto kusema ukweli wawili wa kike na kiume wote kwa mwanamke mmoja, mimi ningetamani amuoe huyo huyo kwa sababu tayari nina wajukuu wawili lakini uamuzi ni wake kanizaa mimi na kamzaa mama yake” Baba Samatta
Mbwana Samatta akiwa na nahodha wa wake wa KRC Genk Thomas Buffel
Je vipi una mfahamu Wema Sepetu na je una mkubali?
“Wema namjua vizuri sana kumkubali kivipi? kwa kazi zake au kivipi kuwa mke wa Samatta? hahahhahah kwanza mimi sijui au inawezekana Wema Sepetu ni mkubwa kuliko Samatta na mimi sipendi mke awe mkubwa ki umri kwa samatta lakini mambo ya ndoa hayo nampa uhuru mwenyewe ataamua”>>>Baba Samatta

Post a Comment

 
Top