Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


KATIKA kile kinachoonekana mambo bado hayapo sawa, majaliwa ya straika Diego Costa yanazidi kuwa tata kutokana na matukio yanayoendelea ndani ya klabu hiyo.
Juzi wafanyakazi wa Chelsea walilazimika kulitoa gari la Costa lililokuwa limeeg-eshwa kwenye eneo la magari ya wachezaji wa kikosi cha kwanza na kulipeleka kwenye eneo la wachezaji vijana wanapoegesha magari yao.
Costa alirejea klabuni hapo hivi karibuni baada ya kuwa nje ya England licha ya msimu kuanza kutokana na kutofautiana na kocha wake, Antonio Conte.
Mabosi wa Chelsea waliagiza gari hilo aina ya Range Rover kuondolewa alipokuwa ameliegesha na kulihamisha kwenye ile sehemu ya vijana ili kumfanya kutojichanganya na wenzake wanaocheza kikosi cha kwanza.

Post a Comment

 
Top