Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Msanii wa muziki Bongo, Alikiba amedai sababu ya ngoma yake ‘Seduce Me’ kupokelewa vizuri hadi kugusa viongozi mbali mbali wa kisiasa ni sababu ya yeye kutengeneza muziki mzuri.
“Muziki mzuri ukitoa kila mtu anaukubali haijalishi kwamba huyo ni kiongozi au mheshimiwa watu wanasikiliza muziki kwa sababu ni sehemu ya maisha yao,” ameiambia Dj Show ya Radio One na kuongeza.
“Nimefurahi sana kwa kweli na jinsi muziki umetanuka na kufika mbali. Inaniongezea nguvu ya kufanya kazi nzuri ambayo nahisi itaizidi kuipeleka Tanzania yetu mbele kutangaza lugha ya Kiswahili,” amesisitiza.
Ngoma ya Seduce Me ilitoka August 25 mwaka huu na hadi sasa ina views milioni 4.6 katika mtandao wa YouTube.

Post a Comment

 
Top