Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Aika.
MWANADADA anyeunda kundi la Muziki la Navy Kenzo, Aika amefunguka kuwa suala la wasanii kuwa na makundi wanayoyaita timu zao halimuumizi kabisa kichwa na wala ni jambo zuri kwani linawagawa wasanii badala ya kuwajenga na kuwafanya kuwa kitu kimoja.
Akipiga stori na Showbiz, Aika alisema kuwa kundi lake linafanya muziki wa watu wote na halina muda wa kugawa kuhusu timu na anawashangaa wanamuziki wenye timu akiwemo Ali Kiba.
“Navy Kenzo na mambo ya timu hatutaki kabisa kuyasikia maana zaidi ya kujenga yana bomoa. Unajua unapokuwa na timu automatic unawagawa mashabiki wako jambo ambalo binafsi naliona si zuri kwa mwanamuziki,” alisema Aika.

Post a Comment

 
Top