Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail ThisChuki na visasi bado vimetawala kwa mastaa wakubwa wawili waliokuwa marafiki wa sinema za kibongo, kajala Masanja ‘kay’ na Wema isaac Sepetu baada ya kila mmoja kurusha kombora kwa mwenzake na kuonesha wazi kuwa bado kuna visasi kati yao ambavyo haviwezi kumalizika kirahisi na pengine hadi kifo.

MTU WA KARIBU Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa wawili hao ambao urafiki wao ulitengeneza historia, kutoonekana mahakamani kwa Kajala katika kipindi ambacho Wema amekuwa akisota kwa msala wa matumizi ya madawa ya kulevya, kulisababisha
mwanamama huyo kuonekana ana roho mbaya.

MAHAKAMANI Kisutu Ilisemekana kwamba, hali hiyo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara hasa Wema anapokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar ambapo marafiki zake husikika wakipaza sauti za kumtusi Kajala ambaye wakati yeye ana msala mahakamani, Wema alikuwa hakauki kufika na kumfariji.


“Mara zote ambazo Wema amekuwa akihudhuria mahakamani kutokana na kukabiliwa na kesi yake ya kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake, Kajala hakuwahi kuonekana hata mara moja kuonesha kumpa sapoti kama yeye alivyokuwa akifanya wakati Kajala akiwa Segerea.


Kutokana na kutoonekana huko mahakamani, Kajala aliwahi kufunguka kuwa anaumia sana kumuona Wema mahakamani, lakini alishindwa afanye nini kwa kuwa alijua fika kuna watu watakuwa hawamuelewi,” kilifunguka chanzo hicho.


KAJALA ANASEMAJE?
Kwa upande wake Kajala alipozungumza na Ijumaa Wikienda alijibu shombo ambazo amekuwa akizipokea kuhusu Wema ambapo alikuwa na haya ya kusema:


“Ni kweli hakuna kitu kinachoniuma kama ninapomuona Wema mahakamani, lakini kuna wakati ninashindwa nifanye nini kwa sababu sielewi nikifika pale mahakamani nitapokelewa vipi kutokana na maneno ambayo yapo,” alisema Kajala. Staa huyo aliendelea kufunguka kuwa, pale mahakamani kunakuwa na familia nzima ya Wema pamoja na wapambe wake hivyo huwa anapata hofu kuwa atakapokwenda watamchukuliaje kwa kuwa tangu huko nyuma walimuona mtu wa tofauti.


“Jamani mimi ninafikiria sana mara mbilimbili, hivi nitakapofika mimi pale mama yake au ndugu zake watanichukuliaje kwa sababu tangu huko nyuma waliniona ni mtu mwenye roho mbaya sana,” alisema Kajala akionesha kuwa hali ni tete kati yake na Wema.


WIKIENDA NA WEMA Katika mahojiano maalum ya Ijumaa Wikienda na Wema juu ya uhusiano au
urafiki wake na Kajala, mwanadada huyo alifunguka kuwa katika kichwa chake hajawahi kumkumbuka Kajala. “Yaani sitaki kuwa mnafiki, sijawahi kumkumbuka


Kajala hata mara moja,” alisema Wema. Pia Wema aliwahi kuandika ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Snap Chat akimtakia heri ya kuzaliwa Kajala na kuandika maneno haya: “Huko nyuma nilijua nina rafiki kumbe.... Happybirthday K.”


URAFIKI WA KUSHIBANA
Urafiki wa Wema na Kajala ulikuwa ni wa kushibana mno ambapo Kajala alipopata msala wa utakatishaji wa fedha kisha kuhukumiwa kwenda jela miaka mitano au faini ya shilingi milioni 13, Wema alimlipia fedha hizo na kuachiwa huru hivyo baadhi ya mashabiki kuamini kwamba huu ndiyo muda mwafaka wa kulipa fadhila hiyo. Urafiki wa Wema na Kajala uliota mbawa baada ya wawili hao kutuhumiana kuchukuliana mabwana.

Post a Comment

 
Top