Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Malkia wa filamu Bongo na Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Sepetu amefunguka iwapo atakuja kusimamia tena wasanii wa muziki kupitia menejimenti hiyo.
Endless Fame kipindi cha nyuma ilikuwa ikisimamia wasanii wa Bongo Flava kama Mirror na Ally. Katika red carpet ya uzinduzi wa filamu yake ‘Heaven Sent’, Wema amesema sasa amejikita katika kusimamia vipaji vipya katika uigizaji na sio muziki.Hapana sitoweza kufanya nao kazi tena ni watukutu sana, nimeona kumeneji wasanii is too much work acha mimi nitameneji wasanii wangu wapya,” amesema Wema.Kwa hiyo nitaangalia wale wenye vipaji vipya lakini wanajua kazi tofauti na ukichukua watu mastaa halafu wengine hawajui kuigiza wapo ili mradi wapo, kuna watu wengi wana vipaji lakini hawajui platform ya kuanzia,” ameongeza.

Post a Comment

 
Top