Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na wanahabari.
Mkuu wa Kikosi cha Maji wa China (Navy), Shen Hao, akielezea ujio wao hapa nchini.

Baadhi ya viongozi wa China wakiwa katika hafla hiyo.
Wakiwa katika picha ya pamoja.
VIONGOZI wa jeshi la China leo wamemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ambapo amewaomba kumsaidia kuwapatia vifaa vya kutumiwa na askari wa doria katika Bahari ya Hindi ili waweze kukabiliana na wahalifu wenye kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Makonda ameeleza kuwa ujio wa viongozi hao umejadili pia masuala mengi ya ushirikiano baina ya watu wa nchi hizi mbili na kuhakikisha usalama wa wao na ushirikiano mwingine wa nyanja mbalimbali.

Naye Mkuu wa Kikosi cha Maji cha China (Navy), Shen Hao, amepongeza juhudi za mkuu huyo wa mkoa hasa za kuhakikisha anapambana na watu wanaoingiza madawa ya kulevya wakipitishia pembezoni mwa Bahari ya Hindi na akasema ushirikiano wa nchi yake na nchi ya Tanzania utaendelea kuwa imara.

Stori: DENIS MTIMA/GPL

Post a Comment

 
Top