Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Ni Mbunge kutoka Nzega vijijini ambae pia ni Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangalla na Mbunge Chalinze Ridhiwani Kikwete kwenye hii post ambapo ishu imeanzia kwenye alichopost Dr. Kigwangalla.Aliweka picha ya vijana wa Kitanzania wakionekana kupambania kupata kazi TRA ambapo iliripotiwa kwamba nafasi za kazi zilizotangazwa na TRA ni 400 lakini waliojitokeza ni zaidi ya elfu 30.
Sasa baada ya kuiweka hiyi picha Dr. Kigwagalla aliandika “Je, hii inaashiria ukubwa wa tatizo la ajira nchini ama ni kwamba watu wetu wanachagua sana kazi za kwenda? #NjeyaBox”

Baada ya picha hiyo kupostiwa kwenye Twitter ya Dr. Kigwangallabaadhi ya Watanzania walitoa maoni yao ambapo miongoni mwao ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete aliemuandikia >>> “Unaweza dhani unauliza swali kumbe nawe unakua sehemu ya wachochezi! Mh. Waziri unaweza kuwa hujui kusoma lkn picha inatoa jibu sahihi”

Post a Comment

 
Top