Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Lebron James
NBA wametangaza ratiba ya Ligi yao ya msimu wa 20172018, ambayo itarushwa na vituo vitatu vya televisheni TNT, Kwese Sports na ESPN. Hii ni ligi ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mchezo wa kikapu kutokana na umaarufu wake na ubora wa wachezaji wanaoshiriki ligi hiyo.
Mashabiki wanawasubiri mastaa kama Lebron James na Steven Curry kama watapata nafasi ya kuendelea kuonyesha umwamba wao msimu huu. Hata hivyo, maombi ya timu nyingi ya kuwa na mapumziko kipindi cha Sikukuu ya Krismasi yaani Desemba 25 na 26, yametupwa na sasa siku hiyo kutakuwa na mechi tano ambapo tatu zitaonyeshwa Live na mbili zitarekodiwa.
Mchezo ukiendelea.
Raha inarejea tena kwa mashabiki waliokuwa wanatazama mchezo wa kikapu kupitia TV1 ambao chaneli waliyokuwa wakitumia msimu uliopita ya Kwese Sports, ambayo ni maalum kwa kurusha mchezo huo Afrika itaendelea kutoa burudani kwa mechi zote kubwa Live. Mechi za msimu huu zinatarajiwa kuanza Oktoba 17, ambapo hadi Oktoba 20 timu 14 zitakuwa zimeshacheza mchezo mmojammoja.
Sherehe hizo zitaanza tarehe hiyo kwa mabingwa watetezi Golden State Warriors kutambulisha kombe lao walilotwaa msimu uliopita kwa mashabiki wao na baadaye watakawaribisha Houston Rockets ambao watakuwa na staa wao mpya Chris Paul, ambaye atacheza mchezo wake wa kwanza na timu hiyo. Paul anapewa nafasi kubwa ya kufanya maajabu kwenye msimu huu kwa kuwa ni kati ya wachezaji bora zaidi kwenye kipindi cha NBA
kilichopita.
Pia staa Gordon Hayward, anatarajiwa kuitumikia timu yake Boston Celtics kwenye mchezo wake wa kwanza wakati itakapovaana na mastaa waliofika fainali msimu uliopita, Cleveland Cavaliers. ESPN msimu huu watakuwa wakionyesha michuano ya NBA, kwa mara yao ya 16 wakitajwa kama televisheni ambayo imekuwa ikionyesha mchezo huu kwa mafanikio makubwa zaidi na sehemu kubwa ya dunia
Wengine ukiachana ESPN na Kwese ambao watakuwa wakionyesha michuano hiyo kwa upande wa Afrika, TNT nao ni kampuni ambayo inapewa nafasi kubwa ya kuwika ikiwa inatajwa kuwa itaonyesha mchezo wa kwanza wa NBA kati ya Oklahoma City Thunder ambayo itakuwa na staa wake Paul George ambao watawakaribisha New York Knicks, lakini pia wataonyesha mchezo kati ya LA Clippers watakaovaana na Los Angeles Lakers kwenye mchezo wao wa pili. NBA, wametangaza kutakuwa na michezo mitano siku ya tarehe 25 Desemba, ikiwa ni mwaka wa kumi mfululizo, lakini kwa mara ya kwanza ABC watakuwa wakionyesha michezo mitatu Live.

Post a Comment

 
Top