Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Taarifa zilizopo kwa sasa katika mitandao ya kijamii duniani kote na vyombo vya habari vya Ulaya ni kuhusiana na ishu ya mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona Neymar kuhusishwa kukaribia kujiunga na Paris Saint Germain ya Ufaransa.
Habari kutoka katika mitandao mingi ya Ulaya inaripoti kuwa PSG hadi sasa wana asilimia 90 ya kumpata Neymar kutokana na mchezaji huyo kuiomba na kuishinikiza Barcelona imuuze, baada ya kocha kumpa ruhusa Neymar na FC Barcelona kuthibitisha Neymar kuombwa kuuzwa.
Lionel Messi ambaye amecheza na Neymar kwa miaka minne toka staa huyo ajiunge na Barcelona, ametumia ukurasa wake wa instagram kumtakia kila la kheri Neymar ambaye leo inaaminika ameshasafiri kuelekea Pariskukamilisha uhamisho huo.
“Ilikuwa ni heshima kushea chumba kimoja cha kubadilishia nguo na wewe kwa miaka yote hiyo rafiki yangu Neymar kila la kheri katika hatua mpya ya maisha yako”>>>Messi

Post a Comment

 
Top