Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Salome Urassa ‘Thea’.
SIKIA hii. Staa ‘mhenga’ katika tasnia ya uigizaji Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ amesema kuwa, anaendelea kukua katika maadili bora kufuatia malezi ya wazazi wake husasan baba yake ambayealimuwekea misingi ya nidhamu na alipokengeuka alidhibitiwa kwa fimbo hata alipokuwa mama.
Katika kubadilishana mawazo juu ya maisha na mwandishi wetu hivi karibuni, Thea ambaye ni miongoni mwa wasanii wa kike watulivu, alisema kuwa, nyumbani kwao kuna kanuni na tamaduni za kikoloni hivyo hakuna mtoto aliyekua hana maadili na misingi bora ya maisha.
“Weee! Baba yangu alikuwa kiboko, mimi mwenyewe nilikuwa napigwa fimbo na ukubwa wangu huu, nakumbuka kuna siku nilikwenda kumtembelea rafiki yangu, tena si miaka mingi sana, lakini nililala huko bila ruhusa ya wazazi, niliporudi kesho yake, nilishushiwa kichapo cha mbwa koko, kwa hiyo niko hivi nilivyo kwa sababu ya malezi bora ya baba yangu hususan fimbo zake,” alisema Thea.

Post a Comment

 
Top