Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Msanii wa muziki kutoka label ya WCB, Harmonize ametua nchini Nigeria kuweka kambi kwaajili ya kurekodi kazi yake mpya ambayo inadaiwa itakuwa ni kolabo.Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Sina’ alisafiri mapema wiki hii akiwa na bosi wake, Sallam.

Harmonize ameonekana akiwa studio akirekodi wimbo huo chini ya producer, Krizbeatz ambaye tayari ana hits kibao mtaani ikiwemo, Pana ya Tekno.
Harmo ambaye anatarajia kupata mtoto na mzungu wake Sarah, ameonekana katika picha mbalimbali akiwa studio na mtayarishaji huyo hodari wa muziki.

Post a Comment

 
Top