Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

                         MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUTENGENEZA POMBE ZA (VIROBA) KIENYEJI NA KUZIHIFADHI KWENYE VIFUNGASHIO VYA CHUPA ZA PLASTIKI KIASI CHA BOKSI 33, WILAYANI NYAMAGANA.MAJAMBAZI WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA NA UPORAJI WA FEDHA WILAYANI ILEMELAKWAMBA TAREHE 01.08.2017 MAJIRA YA SAA 16:35HRS JIONI KATIKA MTAA WA NYANZA KATA YA MKOLANI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, DEUS CHACHA, MIAKA 29, MKAZI WA MTAA WA NYEGEZI, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUTENGENEZA KIENYEJI POMBE ZILIZOHIFADHIWA KWENYE VIFUNGASHIO VYA PLASTIKI MAARUFU KAMA VIROBA ZENYE KATAZO LA SERIKALI KIASI CHA BOKSI 33 AINA YA PAMA DRY GIN, AMBAZO ALIZIJAZA KATIKA VICHUPA VINDOGO VYENYE UJAZO WA MILILITA 100 HADI 200 KISHA KUZIPA JINA LA BLUE SKY NA KUWEKA NEMBO YA TRA TAYARI KWA KUUZWA MTAANI, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI NA KINYUME NA TARATIBU ZA UTENGENEZAJI WA VILEO.

                                              
AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA KATIKA MAENEO YA NYANZA – MKOLANI, YUPO MFANYABIASHARA MWENYE KIWANDA BUBU KINACHOTENGENEZA POMBE ZINAZOHIFADHIWA KWENYE MIFUKO YA PLASTIKI MAARUFU KAMA VIROBA KISHA HUWAUZIA WATU WA HAPO MKOLANI NA MAENEO JIRANI HUKU VIROBA HIVYO VIKIWA NA NEMBO YA TRA.

POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA MAOFISA WA TRA WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI MAENEO TAJWA HAPO JUU KISHA MSAKO NA UPELELEZI WA KUMTAFUTA MTU HUYO ANAYEDAIWA KUFANYA BIASHARA HIYO HARAMU YA POMBE ZA VIROBA ULIENDELEA. AIDHA WAKATI ASKARI WANAENDELEA NA UPELELEZI MAENEO HAYO WALIWEZA KUBAINI MAHALI ANAPOISHI MTUHUMIWA NA KUFANIKIWA KUMKAMATA HUKU AKIWA NA BOKSI HIZO ZA POMBE ZA VIROBA.

POLISI WAPO KATIKA UPLELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA MSAKO WA KUWATAFUTA WAFANYABIASHARA WENGINE WANAOSHIRIKIANA NA MTUHUMIWA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA BIASHARA HIYO HARAMU YA POMBE ZA VIROBA BADO UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWAOMBA WATOE USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI PALE WANAPOONA AU KUBAINI KUWEPO KWA WATU WANAOFANYA UHALIFU KAMA HUU, KWANI VITENDO HIVI VINAHATARISHA AFYA ZA WATUMIAJI LAKINI PIA KUKOSESHA SERIKALI MAPATO.

KATIKA TUKIO LA PILI;

KWAMBA TAREHE 19.07.2017 KATIKA MKOA WA SINGIDA WALIKAMATWA MAJAMAZI WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.SEIF WAZIRI @ CHEMKA MIAKA 37 NA 2.DAUD KAINI MWAKALINGA MIAKA 35, WOTE WAKAZI WA DODOMA, WAKIWA NA FEDHA KIASI CHA MILIONI 2,000,000/= NA DOLLA ELFU 20 PAMOJA NA KUPATIKANA KWA SILAHA AINA YA SHORTGUN YENYE NAMBA 011765714 NA CAR NAMBA 00107210, VITU AMBAVYO WALIPORA HAPA MKOANI MWANZA MAENEO YA KISEKE “A” HII NI BAADA YA KUVAMIA KAMPUNI YA WEISH .A.S.T. LTD AMBAYO INAJIHUSIHA NA BIASHARA YA MABONDO NA KUPORA FEDHA KIASI CHA TSH 40, 000,000/= NA DOLLA LAKI MOJA NA ELFU TISINI PAMOJA NA SILAHA AINA YA SHORTGUN, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

TUKIO HILO LA UPORAJI NA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA LILITOKEA TAREHE 14.07.2017 AMBAPO MAJAMBAZI HAO WAPATAO WATANO WALIVAMIA KIWANDA HICHO TAJWA HAPO JUU HUKU WAKIWA NA MAPANGA, MAWE NA NONDO KISHA WAKAMPIGA MLINZI NA KITU KIZITO KICHWANI NA KUFANIKIWA KUMPORA SILAHA ALIYOKUWA NAYO AINA YA SHORTGUN NA KUFANIKIWA KUINGIA NDANI YA KIWANDA HICHO KISHA WALIWAJERUHI WAMILIKI WA KIWANDA HICHO NA KUPORA KIASI HICHO CHA FEDHA NA SILAHA NA KUKIMBIA MAENEO YASIYO JULIKANA.

AIDHA BAADA YA TUKIO HILO KUTOKEA POLISI WALIPOKEA TAARIFA HIZO NDIPO UFUATILIAJI NA MSAKO WA KUWATAFUTA MAJAMBAZI HAO KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA MKOA WA MWANZA NA MAENEO YA MIKOA JIRANI ULIANZA. AIDHA WAKATI MSAKO UNAENDELEA ASKARI WALIPOKEA TAARIFA ZA KIINTELEJENSIA KWAMBA MAJAMBAZI HAO WAMEKIMBILIA MKOANI SINGIDA NDIPO ASKARI WALIKWENDA HADI MKOANI HAPO NA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA MKOA WA SINGIDA NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA MAJAMBAZI HAO WAWILI .

KATIKA MAHOJIANO YA AWALI NA ASKARI BAADA YA KULETWA MWANZA, MAJAMBAZI HAO WALIKIRI KUHUSIKA KATIKA TUKIO HILO KISHA WALIONESHA MAHALI WALIPOKUWA WAMEIFICHA SILAHA NA KUMTAJA MWENZAO MWENGINE AMBAYE TAYARI AMEKAMATWA AITWAYE EMANUEL MWAKILILI MKAZI WA MKAZI WA DODOMA NA DAR ES SALAAMU. POLISI WAPO KATIKA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE WA TATU, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE WATATU WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA MSAKO WA KUWASAKA MAJAMBAZI WENGINE WAWILI AMBAO BADO HAWAJAPATIKANA UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUWA WATULIVU HUKU WAKIENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU MAPEMA ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.

IMETOLEWA NA;

DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Post a Comment

 
Top