Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mafahari wawili wakishindana zinazoumia ni nyasi. ‘Sedece Me’ na ‘Ziipendwa’ zazidi kupigana vikumbo katika Mtandao wa YouTube.
Ngoma ya ‘Sedece Me’ yarudi kwenye kiti chake cha namba moja trending kwenye mtandao huo baada ya kupokonywa nafasi hiyo kwa masaa kadhaa na wasanii wa WCB kupitia wimbo wao mpya, Zilipendwa.
Alikiba kupitia wimbo wake huo alikaa katika nafasi hiyo ya uongozi kwa siku tano huku wimbo huo ukiwa umetazamwa zaidi ya mara 2.5 milioni huko YouTube kabla ya kushushwa Jumatano hii na wimbo wa ‘Zilipendwa’ wa WCB ambao nao walionja kukalia kiti hicho kwa masaa machache na kurudisha kijiti kwa aliyekuwa nacho.
Mpaka sasa ‘Seduce Me’ tayari umejitengenezea rekodi kadhaa kwenye mtandao huo ikiwemo kufikisha views milioni moja ndani ya masaa 38.

Post a Comment

 
Top