Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Rais Paul Kagame akishangilia ushindi.
Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda imemtangaza Paul Kagame kuwa mshindi wa urais wa nchi hiyo katika uchaguzi uliyofanyika jana Ijumaa, Agosti 4.Tume hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais huyo ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 17 sasa, atahudumu muhula wa tatu wa miaka saba baada ya kushinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa.
Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa kuonyesha utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuaawa.
Kutoka kushoto Paul Kagame, Frank Habineza na Philippe Mpayimana.
Wapinzani wa Kagame walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana ambao amewaburuza vibaya kwenye matokeo hayo ambapo wapinzani hao wamelalamika kuwa wafuasi wao wamepigwa zengwe ndiyo maana imesababisha kuwepo watu wachache katika mikutano yao ya kabla ya kura. Hata hivyo chama tawala kimekana madai hayo.
Rais Kagame aliingia madarakani mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi lilichukua udhibiti wa mji mkuu Kigali na kukomesha mauaji ya kimbart ambapo watu 800,000 watusi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.
Katiba ya Rwanda ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2015 na kumpa Kagame fursa ya kusalia madarakani hadi mwaka 2034.

Post a Comment

 
Top