Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Neymar amewasili Portugal na ndege binafsi kwaajili ya kufanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na klabu ya PSG kwa ada ya pauni milioni 198 kiasi ambocho kinamfanya kuweka rekodi ya dunia akitokea Barcelona.Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili amewasili Porto usiku wa Jumatano mara baada ya kuuwambia uongozi wa Barca kuwa anahitaji kuondoka na kujiunga na matajiri wa Ufaransa PSG kwa dili ambalo litamuhakikishia kulipwa pauni 500,000 kwa wiki.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, hakufanya mazoezi na Barcelona siku ya Jumatano na amepatiwa ruksa ya kuondoka katika klabu hiyo.Mtandao wa Barcelona umetoa maelezo kuwa “Neymar Jr, akiwa na Baba yake na wakala wake wamethibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo baada ya kukaa kikao na ofisi za klabu hiyo.

Post a Comment

 
Top