Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MWANAMAMA aliyewahi kuwika miaka ya nyuma kunako tasnia ya filamu Bongo, Lucy Komba, amejikuta akipoteza sifa ya mwanamke mvumilivu baada ya kutoa povu kwenye ukurasa wake wa Instagram, chanzo kikiwa ni Hamisa Mobeto.
Nyongo ya mwanamama huyo ilitibuka baada ya kuona baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii wakimshambulia kwa maneno Hamisa Mobetto, kuhusiana na mtoto aliyejifungua hivi karibuni, hali iliyompelekea kukumbuka vichambo alivyowahi kuvipokea kuhusiana na ndoa yake.

“Samahani lakini kimenichoma, Mabogas ya TZ yanamponda Mtanzania mwenzao, yanamsifia Bogas, sijui yanadhani yatapewa ule urithi, mbona Waganda hawambabaikii? Acheni umaskini wa kujirahisisha. Au mnafikiri mtapitishiwa kila mmoja karanga mojamoja ya bure?”
Na baada ya posti hiyo akaona haitoshi muda mfupi baadaye akaposti tena picha ya Hamisa akiwa na mtoto wake wa kwanza, Fantasy, na kuandika maneno yafuatayo:


“Hongera mwanamke mwenzangu, wanajifanya roho ngumu tu kukuponda wakati roho zinawauma, unatoa vitu hasa mwanamke unazaa huku unatabasamu, wale wanaoniponda ningekuwa mzalendo nisingeolewa na Mzungu;
“Ndiyo nimeolewa na Mzungu sababu sina ubaguzi wa rangi wala ukabila na tangu nimeolewa sijawahi kutukana kaka zangu wa Kiafrika, kwa hiyo lazima mjue kutofautisha A na B;


“Pili anayewapa taarifa nimeachwa nahisi kama kachelewa kuwataarifu halafu mwambieni awape taarifa kamili maana huwa anaingia Insta na kuzizungusha bado hajawapa taarifa za kunichamba;
“Ukweli unauma mmepewa ukweli kwa huyo mgeni wenu aliyenenepesha miguu, kiuno kimeshindikana kukipunguza mnalia, chambeni tu mniongezee Followers maana nilikuwa sijaamka bado kujua kumbe umaarufu wa Bongo unatokana na vichambo” ameandika Lucy Komba.

Post a Comment

 
Top