Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Msanii wa Harmorapa ameshindwa kunyoosha maneno iwapo kweli amegombana na P Funk hadi kumchana katika ngoma yake mpya.
Tetesi zilizopo ni kwamba menejiment ya Harmorapa ilishindwa kuafikiana na P Funk baada ya msanii huyo kupata dili kutoka kampuni moja ya vinjwaji ambapo inakadiriwa dili hiyo ilikuwa Tsh. Milioni 100 kitu ambacho Harmorapa amekikanusha.Sitaki nizungumzie sana kama ile milioni 100 nimepigwa au lah!. Kiukweli sipo naye tofauti sana ila kwa sasa hivi sina naye mawasiliano, siku zote kuna kupishana,,, mimi sijui kama alikuwa anakula maslai yangu,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio.
Alipoulizwa kuhusu kumchana Majani katika ngoma yake mpya ‘Ajitokeze’ alisema “sijamaanisha majani kama majani, nyimbo yenyewe inahusisha maisha, kwa mfano mimi nafanya kazi kwa mtu halafu mwisho wa siku ile kazi maslai inakua juu yake” amesema na kuongeza.
“Kwa mfano nafanya kazi kwa jasho najituma halafu pesa yangu siioni au kunufaika mwisho wa siku yule ambaye alikuwa ananufaika anakuona haufai” ameongeza.

Post a Comment

 
Top