Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva nchini Dully Sykes amefunguka na kutaja wasanii watano ambao kwa mtazamo wake yeye anaona watadumu muda mrefu kwenye muziki na midomoni mwa watu hata kama hawatakuwa na nyimbo zozote hewani.

Dully Skyes akiwa aliwataja wasanii hao kuwa ni pamoja na Alikiba, Mr Blue, Young Dar es Salaam na Diamond na kusema watu hawa jinsi ambavyo wanaishi na kufanya mambo yao kila siku katika maisha ya kawaida lakini watu huyapokea kama mambo makubwa na kuanza kuyafuata, hivyo kwa namna hiyo wasanii hawa wataendelea kuwepo midomoni mwa watu kila siku.

"Wasanii hawa jinsi ambavyo wao wenyewe wamekuwa wakijiweka katika maisha yao ya kila siku wanakuwa gumzo, Alikiba ni maisha yake yale kuvaa sijui vipensi vikali na kila anachofanya kuna watu wanataka kufanya, Diamond amekuwa mtu wa kutupia sijui raba kali na maisha hayo hivyo kuna watu ambao wanapenda hayo maisha yake, ukija huku kwa Young D amekuwa na life style yake ni mtu wa mapicha picha sana na kila anachoweka watu hukizungumzia, lakini ukija kwa Blue ule muonekano wake wa kila siku unafanya azidi kuzungumziwa, hivyo wasanii hawa wanaweza kuwa na kazi au kutokuwa na kazi hewani lakini wakaendelea kuongelewa siku zote" alisema Dully Skyes
Mbali na hilo Dully Skyes alisema kuna wasanii wengi wamekuwa wakipotea kwenye muziki kutokana na kutokuwa na nidhamu ya kazi pamoja na heshima, wamekuwa wakiwadharaua watu ambao wamewafanya kuwa wakubwa na kufika sehemu ambazo wapo kisanii, hivyo aliwataka wasanii kuwa na heshima katika kazi na kuwaheshimu watu ambao wameweza kuwapigania mpaka wakawa wakubwa katika sanaa.

Post a Comment

 
Top