Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Staa wa Bongo Fleva, Msami Baby, anayetamba na kibao chake kipya cha So Fine, alichomshirikisha rapa machachari, Chemical amefungukia taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa, Irene Uwoya, alimtongoza.
Msami ambaye amevunja amri ya 6 na staa huyo wa Bongo Muvi kwa takribani miaka miwili, amefunguka kama ifuatavyo:
“Ni kweli tulikuwa wapenzi kwa muda wa miaka miwili, ila swali la nani alianza kumtongoza mwenzake hilo halina umuhimu hivyo siwezi kuliongelea.
“Kwa mara ya kwanza tulikutana lokesheni kwa ajili ya kushuti muvi yake ambayo ilinihitaji kutokana na uwezo wangu wa kucheza, hapo ndipo mahusiano yetu yalipoanzia, na mpaka sasa hakuna aliyewahi kumtamkia mwenziye kwamba amemuacha, tuliachana hewanihewani tu.”

Post a Comment

 
Top