Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto Jumamosi hii akiwa katika hotel ya Serena Hotel jijini Dar es salaam amekutana na muimbaji mkongwe wa muziki kutoka nchini Africa Kusini, Yvonne Chakachaka.Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Kitendawili, ameonekana akifanya mzungumzo na muimbaji huyo mkongwe.

Meneja wa Mrisho Mpoto, Steve akisalimiana na Yvonne Chakachaka

“Usifanye jambo tu kwakua liko mbele yako au umkomoe fulani, fanya kwakua ulipanga kulifanya na lina baraka za Mungu, #nchiyangukwanza #menginebaadae linazidi kupata baraka za Majirani Wa Africa nzima #ivonchakachaka #done,” aliandika Mpoto Istagram.
Ujumbe huo umezua maswahi mengi mtandaoni huku wengi wakihisi labda ameingia kwenye vuguvugu la Diamond na Alikiba.

Hata hivyo haikujulikana moja kwa moja ujumbe huo unaenda kwa nani.


Post a Comment

 
Top