Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Baada ya kufunga pingu za maisha na kuishi pamoja kwa takribani miaka mitano, kisha kutengana na kila mmoja kushika 50 zake, hatimaye mke wa mwanamuziki, Barnaba Classic, anayejulikana zaidi kwa jina la Zuu, ameibuka na kuanika sababu zilizosababisha kuvunjika kwa ndoa yao, ikiwemo yeye kukosa furaha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuu ameposti picha akiwa na mpenzi wake wa sasa na kuandika ujumbe ufuatao.
“Ni watu wachache sana wanaojua ni kitu gani nilikuwa nakosa katika maisha yangu, unaweza ukapata kila kitu katika maisha ila ukakosa furaha, amani na heshima, kwa zaidi ya miaka mitano, hiki ndiyo nilichokuwa nakitafuta, amani ya moyo”Baaya ya kuposti ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa Istagram, muda mfupi baadaye, akaufuta.
Katika miaka yao mitano ya ndoa, Zuu na Barnaba wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Steve. Tangu kuvunjika kwa ndoa hiyo Barnaba hajawahi kumuweka wazi mpenzi wake mwingine, Huku Zuuakiendelea kutanua na mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva anayeitwa Brown.

Post a Comment

 
Top