Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Staa wa kike wa Bongofleva Nandy amefunguka kueleza siku ya kwanza kufika Clouds kuongea na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akisema Mkurugenzi huyo alimvunjia CD zake mbele ya macho yake.
Nandy amesema”Nakumbuka Boss Ruge wakati ndiyo naenda pale Clouds kwa ajili ya kuongea naye nikiwa nimetoka kwenye mashindano ya Tecno alinambia nimpelekee kazi zangu. Kwa shahuku nikapeleka kazi zangu, nakumbuka alinivunjia CD zangu mbele yangu.
“Alisikiliza na kuzivunja CD kisha kuweka kwenye dustbin akaniambia upo tayari kuanza upya? Yes nipo tayari. Akaniuliza tena unaniamini? Nikamwambia ndiyo nakuamini. Iliniuma sana lakini niliamua kumkabidhi maisha ya muziki wangu na matokeo ninayaona. Alinambia nyimbo mbaya wakati mimi nilikuwa naona kati ya CD zangu hizi hii ndiyo itatoka lakini hajakubali hata moja akazivunja zote.” – Nandy

Post a Comment

 
Top