Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Msanii Gigy Money ameonekana kuwa na mtazamo tofauti na ule uliotolewa na msanii wa kike wa siku nyingi kwenye bongo fleva Stara Thomas, na kusema kuwa si kweli malezi yao ndio yanafanya waimbe muziki usio na maudhui.
Gigy Money amesema kuwa muziki wa sasa watu wanafanya kibiashara zaidi, tofauti na ule ambao wao walikuwa wakifanya na kusema kuwa walikuwa wanafanya muziki wa ngonjera.
"Namuheshimu Stara lakini nimpe pole kwa sababu nahisi katika hilo suala hakuwaza sana aliongea tu, siku hizi muziki ujumbe umfikie mtu kwa namna yoyote, na yeye alikuwa anaimba zamani, halafu zamani ilikuwa wanaimba ngonjera mtu anaongea tu, ye alikuwa anaimba nini, angekuwa msanii mkubwa mpaka leo angekuwepo, kwani wangapi walikuwa wanaimba zamani mpaka leo wanaimba", alisema Gigy Money.
Gigy Money aliendelea kwa kusema kuwa wao wanaangalia muziki ambao utafika kirahisi kwa watu na kuuelewa, haijalishi una ujumbe au la, kwani lengo lao kubwa ufike sokoni na wafanye biashara.
"Sasa hivi mtu anaangalia biashara, mziki ni biashara kitu ambacho mtoto anaweza kukariri ndiyoo kitu ambacho mtu mzima anaweza kukariri, lakini mziki ni mzuri, na malezi hayahusiani na nyimbo, msanii ni tofauti na mtu mwengine, siku hizi watu wanaimba kwa brand", alisema Gigy MOney.
Msikilize kwa undani hapa ambapo amefunguka mengi kuhusu wasanii hao wa kike wa zamani akiwemo Lady Jaydee.

Post a Comment

 
Top