Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mwigizaji Tuesday Kihangala ambaye ni mzazi mwenza na Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye kwa sasa yupo kwenye matatizo, amezungumzia hali anayokabiliana na mwigizaji huyo na kuonesha kusikitishwa kwake ingawa wameachana.
Akionesha kuumizwa na hali iliyomkuta Jini Kabula, Tuesday amesema yupo karibu na familia yake na kuwapa ushirikiano kuhakikisha wanamsaidia kwa hali na mali.
”Ni taarifa za kuumiza sana hata mtu yoyote hata kama huna mahusiano naye na siyo mzazi. Inaumiza sana kama binadamu, ingawa sipo Dar es Salaam lakini tuna mawasiliano mazuri wakati akiwa na nafuu na ninawasiliana vizuri na familia yake kuangalia namna gani tunaweza kutatua hili suala. Tulibahatika kuwa na mtoto mmoja toka mwaka 2007 ambapo tulivunja mahusiano.” – Tuesday Kihangala.

Post a Comment

 
Top