Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Uheard ya leo August 2, 2017 inawahusu tena wanandoa wawili Nuh Mziwanda na Nawali wanaodaiwa kutengana kutokana na wote wawili kutokuishi karibu kama awali huku Nuh Mziwanda akidaiwa kurudi kwenye dini yake ya zamani.Gossip Cop Soudy Brown amewatufuta wote waili kusikia upande wao juu ya hizo tetesi zilizopo kwenye mitandao ambapo kwa upande wa Mwanamke (Nawal), yeye amedai ameshaachana na Nuh ambae amerudi kwenye dini yake hivyo hawezi kuwa mumewe tenaNawal amesema “Nuh hamjali mwanae, na pia kuhusu mimi nimeshaolewa…. mtu akirudi kwenye dini yake anakua sio mume wako tena, kwa ufupi sina mume na hakunishirikishachochote”“Kwa sababu siwezi kuondoka kwangu bila sababu na inabidi hayo umuulize yeye, mimi naona ni yeye mwenye makosa kama hivyo karudi kwenye dini yake hamjali mtoto kivipi tena amuone kama nani..?”
“Mpigie simu umuulize miezi mingapi nyuma kashamuona mwanae..? kashantoka nina mume mwingine kwani hamna habari..? mume wangu hataki mambo ya nini nini.” – Nawali
Nuh mziwanda alipopigiwa simu akayazungumza haya…>>>“Anya nilikuwa nae jana kwenye photoshoot ya wimbo wangu mpya na kwenye cover nitakuwa nae, hapo ndio ushangee hata kama sasahivi sipo nae kwasasa yeye yupo kimpango wake asiwe anaongea vitu ambavyo sio vya kweli kwenye media ili mradi kunifanya mimi nionekane vibaya”

Post a Comment

 
Top