Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
JAMAA ambaye ndiye usingizi wa staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed, Ashrafu Uchebe, ameibuka na kumpa ruksa mpenzi wake ya kuvaa nguo za nusu utupu na kuwaambia mashabiki wamuache avae kwa sababu kazi yake inamruhusu.
Akizungumza na Amani, Uchebe alisema kuwa, anawashangaa wanaomwambia ‘baby’ wake huyo hana mavazi ya staha wakati yeye anamuona yupo sahihi.
“Jamani baby wangu wanataka avae dela apande nalo jukwaani wakati mavazi ya kupanda jukwaani yapo? Naomba waniachie malkia wangu kama wanataka na wao wavae,” alisema Uchebe ambaye uhusiano wake na mwanamuziki huyo umekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Post a Comment

 
Top