Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Baada ya msanii Shilole kutangaza kufunga ndoa wakati wowote, naye mchekeshaji kutoka Timamu, Ebitoke amedai kuwa anatarajia kufunga ndoa na mkali wa RnB Bongo, Ben Pol wakati wowote.Ebitoke ameeleza kuwa moja ya malengo yake kwa sasa ni kufunga ndoa na msanii huyu pia kufanya naye kazi kwa ukaribu zaidi.Ben Pol ni mpenzi wangu na yupo katika harakati za kutimiza malengo yangu, ikiwemo kufunga naye ndoa na kufanya kazi naye pamoja na kusaidiana, ila siwezi kusema ndoa itakuwa lini ila ndo kwanza tupo katika malengo na mipango,” amesema Ebitoke.
Akaongeza “Hivyo vitu vitakuja kwa sababu tuna malengo na mipango hiyo kwa sababu yeye ni mwanaume na mimi ni mwanamke.”

Post a Comment

 
Top