Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Pogba na Lukaku wakishangilia kwa pamoja baada ya kuwatupia wapinzani wao siku ya jana.
Manchester United imeendelea kuwa na mwanzo mzuri katika Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ baada ya kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Swansea City.
Kocha wa Swansea, Paul Clement akisalimiana na Kocha wa Man Utd, Jose Mourinho.
Man United sasa imefikisha pointi sita katika michezo miwili na imefunga mabao 8.
Waliofunga mabao katika mchezo huo ni beki Eric Bailly aliyefunga bao lake la kwanza akiwa ndani ya kikosi hicho, straika Romelu Lukaku alifunga bao moja na kumfanya afikishe mabao matatu ndani ya michezo miwili, Paul Pogba na Anthony Martial wakamalizia kazi hiyo.
Wachezaji wa Man wakipongezana kwa pamoja.
Mchezo ujao wa Manchester United utakuwa ni dhidi ya Leicester City kwenye Uwanja wa Old Trafford, Jumapili ijayo.
Pogpa akishangilia baada ya kutupia.
Swansea: Fabianski, Fernandez, Bartley (Routledge 67), Mawson, Roque (Narsingh 67) , Naughton, Fer, Carroll, Olsson, Abraham (McBurnie 82), Ayew.

Subs: van der Hoorn, Nordfeldt, Rangel, Fulton.

Booked: Fer

Man Utd: de Gea, Valencia, Bailly, Jones, Blind, Pogba, Matic, Mata (Fellaini 75), Mkhitaryan (Herrera 85), Rashford (Martial 75), Lukaku.

Subs: Romero, Lindelof, Smalling, Lingard.

Booked: Pogba

Goal: Bailly 45, Lukaku 80, Pogba 82, Martial 84.

Referee: Jon Moss (W Yorkshire)

Attendance: 20,862

Post a Comment

 
Top