Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MAMA mzazi wa mwanamuziki nyota nchini Marekani, Wiz Khalifa, amemfungulia kesi ya udhalilishaji aliyekuwa mkwe wake ambaye ni mwanamitindo Amber Rose.Mama huyo anayeitwa, Katie Wimbush-Polk, amesema kuwa Amber Rose alimtolea kauli za kumtuhumu kuwa ni mama asiyefaa hata kumlea mjukuu wake Sebastian, mhalifu, pamoja na kumhusisha na kifo cha bintiye ambaye ni dada wa Wiz Khalifa.Kutokana na kauli hizo mama huyo amefungua kesi ya madai ya zaidi ya shilingi milioni 100 za Kitanzania, ambapo mpaka sasa Amber Rose hajajibu chochote, wala kuandika chochote kwenye kurasa za mitandao yake ya kijamii.Wiz Khalifa na Amber Rose walifunga ndoa mwezi julai mwaka 2013, na ndani ya ndoa hiyo walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Sebastian.
Miezi michache baada ya mtoto huyo kuzaliwa ndoa hiyo ikavunjika huku ‘uchepukaji’ ukitajwa kuwa chanzo cha yote, na mpaka sasa Wiz Khalifa hajatoa tamko lolote kuhusu mama yake kumfungulia kesi mzazi mwenziye

Post a Comment

 
Top