Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Eneo alilofanyiwa upasuaji.
HUJAFA hujaumbika! Hii ni kauli iliyojaa simanzi ya mwanamama Khadija Abrahmani, mkazi wa Tandale Sokoni jijini hapa kutokana na maradhi ya tumbo yanayomsumbua baada ya kufanyiwa oparesheni tano kisha utumbo kulegea.Akizungumza na mwandishi wetu, alisema, mtoto wake wa kwanza na wa tatu aliyemzaa mwaka 2012, wote aliwazaa kwa oparesheni, baada ya miezi sita alipojifungua mtoto huyo ndipo tatizo la uvimbe tumboni likamuanza sehemu ya mshono.
Akifafanua zaidi huku akionekana kuwa na maumivu makali, mama huyo alikuwa na haya ya kusema:
UVIMBE ULIVYOANZA
“Nilipojifungua mtoto wangu wa tatu baada ya miezi sita uvimbe ukaanza katikati ya mshono, lakini mwanzo ukawa hauumi kwa nje kumbe ndani ulikuwa umeachia, kipindi hicho nilikuwa nipo Mombo, Tanga, ilibidi nifanyiwe oparesheni.
Khadija Abrahmani akijipumzisha.
OPARESHENI YA NNE
“Baada ya kupita miezi mitatu nilipofanyiwa oparesheni hiyo ya nne nikiwa nimehamia Dar na mume wangu, nikaanza kuumwa tena, nilipoenda hospitali wakasema nina kidole tumbo kimepasukia tumboni, nikaenda tena kufanyiwa oparesheni ya tano katika Hospitali ya Mwananyamala.

“Baada ya kupita miezi mitano tangu nilipofanyiwa oparesheni, ile sehemu ya mshono ikaanza kufutuka na wiki iliyopita nikiwa nimejipumzisha sebuleni nikaona maji yanamwagika kutoka tumboni.AGUSA UTUMBO

“Nikagusa na kuona nagusa utumbo, niliogopa sana, nikaingia chumbani kujitazama nikaona vitu vya ndani ya tumbo, nilichanganyikiwa, nikamuita mdogo wangu wa kiume ambaye ndiye ndugu yangu wa pekee hapa Dar na jirani yangu, walipokuja hawakutaka hata kunitazama mara mbili wakaogopa mno.“Kutokana na hali hiyo ikabidi wanikimbize Hospitali ya Tandale, ambapo nilipewa huduma ya kwanza na kutakiwa kwenda Hospitali ya Mwananyamala. Nilipofika huko madaktari walistaajabu na kunihoji kama kuna kitu nilifanya hadi kuwa kwenye hali hiyo, nikawaambia kuwa sehemu hiyo imepasuka yenyewe.

Hakika ni huruma.NIWEKEWE KIRAKA

“Pale Mwananyamala akaitwa daktari ambaye alinifanyia oparesheni ya kidole tumbo, waliponichunguza wakabaini kuwa ngozi imechoka kwa sababu nimeshafanyiwa oparesheni mara nyingi, hivyo imekuwa laini.

“Waliniambia inabidi niwekewe kiraka kinachouzwa shilingi laki mbili na ikiwezekana nisizae tena.OMBI KWAKO MSOMAJI

“Naomba Watanzania wanisaidie fedha za kununulia hicho kiraka, shilingi laki mbili sina na shilingi laki moja za gharama za matibabu pia sina, isitoshe kuna dawa nyingi natakiwa ninunue sina uwezo, mume wangu hana uwezo, napata maumivu makali, nateseka.”

Kwa yeyote aliyeguswa na habari hii anaweza kumsaidia mgonjwa huyu kupitia namba 0783 204 689 ili kufanikisha matibabu yake.

Post a Comment

 
Top