Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wema Sepetu.
ZAMANI maisha ya mastaa wengi wa kike Bongo yalikuwa ni ya mitoko karibu kila siku, usiku kwenda katika kumbi mbalimbali za starehe na kujirusha kwa anasa kama pombe, ngono, kutoka kimapenzi na mapedeshee na nyinginezo. Lakini sasa, mambo yamebadilika, mbwembwe zote zimeisha, wengi wao wanatoka mara moja na wanaozidi ni mara mbili kwa wiki, Amani lina ubuyu ulionyooka.Skendo hiyo inayodadavua kinachoendelea nyumbani kwa baadhi ya mastaa hao wa kike Bongo, ilivujishwa na majirani ‘masnichi’ ambao wanaishi nao beneti akiwemo mwigizaji Wema Isaac Sepetu, Irene Uwoya, Agness Gerald ‘Masogange’ na Aunt Ezekiel.
Masnichi hao waliweka wazi kwamba, kabla ya usawa kukaa vibaya, mastaa wengi walikuwa wakijiachia kwa ngono pombe na kila aina ya anasa huku wakimwaga fedha katika kipindi cha serikali ya awamu ya nne, lakini tangu serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ iingie madarakani, wengi wamejikuta wakiumbuka kwa ukata na kushindwa kutoka.
SNICHI WA KWANZA

“Mimi ninaishi hapa jirani na anapoishi Aunt Ezekiel (Mwananyamala). Sasa hivi hatoki kwenda misele ya usiku kama ilivyokuwa zamani.
Muda mwingi anautumia kushinda nyumbani na kama akiwa na kazi ya kuigiza, huifanya mchana, lakini ikifika jioni tu, anakuwa amesharejea nyumbani. “Kinachoonekana sasa hivi mambo yamebadilika. Wameufyata wenyewe. Unajua zamani kuna mastaa wengi nilikuwa nikikutana nao, walikuwa wanaishi kama miungu watu. “Walikuwa wanaona maisha wameyapatia na hawakujua kuwa ipo siku watashuka, maisha yao kwa sasa wengi wao ni aibu tupu,” alisema snichi huyo huku akiomba hifadhi ya jina.
SNICHI WA PILI

Mara baada ya kupata ubuyu huo, Amani lilianza kuufanyia kazi kwa kuzungumza na snichi mwingine ambaye yupo karibu na mastaa ambaye pia anafanya kazi katika moja ya klabu kubwa maarufu jijini Dar ambaye naye alishibisha ubuyu wa snichi wa kwanza. “Sasa hivi ukweli hawa mastaa wana hali mbaya.
Inasikitisha kuona hata baadhi yao wanagongea bia klabu. Kama hiyo haitoshi, siku hizi hakuna amshaamsha kama zamani. Zamani tulizoea kuwaona klabu kuanzia Jumatatu hadi Jumatatu. “Siku hizi wanakuja kwa nadra sana. Ukimuona mmoja Jumamosi, basi ujue ndiyo mpaka Jumamosi nyingine. Yaani hawana zile za kujiachia kila siku, tena afadhali wa kiume, mastaa wa kike siku hizi ni nadra kabisa,” alishibisha hoja snichi huyo.


MAKACHERO WAWAFUNGIA KAZI

Mara baada ya masnichi hao kumwaga ubuyu huo, ‘makachero’ wa Amani kwa kushirikiana na wale ‘wanajeshi’ wa Kikosi Maalum cha Operesheni Fichua Maovu (OFM), walianza kazi rasmi ya kuwatembelea masnichi wanaoishi jirani na baadhi ya mastaa hususan wale wa kike ambao wametajwa kuathirika zaidi na hali ya uchumi ilivyo sasa.


WA KWANZA NI UWOYA

Makachero wetu walifika nyumbani kwa Uwoya, maeneo ya Sinza-Kwa Remmy, Dar na kufanikiwa kuzungumza na snichi mmoja mbaye ni jirani yake ambapo alifunguka; “Siku hizi kidogo afadhali tangu afungue pub yake ndiyo ameanza kutokatoka, kabla ya hapo ilikuwa tunashinda naye hapa mtaani. Kama unavyoona sasa hivi saa kumi hii jioni, gari lake hilo hapo ndani amepaki tu, kutoka ni nadra sana.”
Uwoya.
KWA WEMA Makachero wa Amani walihamia nyumbani kwa Wema, maeneo ya Ununio jijini Dar ambapo huko alipatikana snichi mzuri ambaye alimwaga mchele kwenye kuku wengi. “Kwa sasa hivi Madam (Wema) hatumuoni akitokatoka kama zamani, maisha yamebadilika sana. Hata zile mbwembwe kama zamani za kufanya sherehe za mara kwa mara, hazipo. Kwa kweli sasa hivi ni heshima na adabu,” alisema snichi huyo.


KWA MASOGANGE

Baada ya hapo Amani lilikita nyumbani kwa mrembo maarufu katika video mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, Masogange anayeishi maeneo ya Makongo, Dar ambapo nako makachero wetu walifanikiwa kumpata snichi mmoja ambaye alifunguka: “Weee sasa hivi Masogange tena atoke usiku? Labda mara moja moja sana. Jeuri ile ya zamani haipo tena. JPM (Rais Maguful) amewanyoosha kwa kweli. Tulikuwa hatunywi maji mjini. Kama anavyosema rais, ni zamu yao kuishi kama mashetani.”
Masogange.
NYUMBANI KWA AUNT

Makachero wetu walifunga kazi hiyo ya kitafiti kwa kufika nyumbani kwa mwigizaji Aunt, maeneo ya Mwananyamala, Dar na kuzungumza na snichi mmoja ambaye aliomba asitajwe jina wala picha kupamba ukurasa wa mbele wa habari hii. “Sasa hivi Aunt kutoka ni mara moja au mbili tu kwa wiki, tofauti na zamani kabla ya Magufuli. Vyuma vimekaza kweli, hawatoki usiku. Aunt alikuwa mara kwa mara akitoka na Moze Iyobo, lakini siku hizi wanasikilizia kama Ijumaa au Jumamosi tu,” alivujisha snichi huyo.

Aunt Ezekiel.
WENYEWE WANASEMAJE?
Jitihada za kuwapata wahusika hao ili waweze kutoa maoni yao kuhusiana na masnichi hao ziligonga mwamba kufuatia simu zao kuita bila kupokelewa. Hata hivyo, Amani lilizungumza na muigizaji maarufu, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambaye alikiri maisha kuwapiga mastaa wengi tu. “Kaka tena hao wa kike wengi wameumbuka. Si unajua walikuwa wanategemea zaidi ‘misheni tauni’, tofauti kabisa na kazi zao, vurugu za bethidei, sifa za kumwaga hela kwenye kumbi sasa hivi hakuna tena,” alisema Dude.

Post a Comment

 
Top