Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina.
KOCHA Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba kutokana na mazoezi anayoendelea kuwapa vijana wake katika kambi yao iliyopo Pemba.Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, timu hizo zitapambana katika mchezo huo kuashiria kufunguliwa kwa msimu mpya ambapo Yanga ikiwa imepiga kambi Pemba, wap­inzani wao Simba wame­jichimbia Unguja.Lwandamina amesema wapo tayari kwa mchezo huo kwani anaona kila siku kikosi chake kinaendelea kuima­rika kutokana na wachezaji wake kufuata kile ambacho amekuwa akiwafundisha.Huku sisi tupo vizuri tu­naendelea na mazoezi kama kawaida, kikubwa ambacho naweza kusema ni kwamba vijana wangu kila siku wa­nazidi kuwa imara na ku­nipa matumaini ya kufanya vizuri dhidi ya Simba.
“Kwa namna siku zina­vyozidi kwenda, naona tupo tayari kwa mchezo huo, wapinzani wetu waje tu tupambane,” alisema Lwandamina.

Post a Comment

 
Top