Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ .
MBUNIFU wa mavazi nchini, Ally Remtullah, ametimiza miaka kumi katika kazi yake ya ubunifu wa mavazi ambapo usiku wa kuamkia leo alifanya sherehe kabambe katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Safari ya ubunifu huo aliianza mwaka 2007 ambapo mteja wake wa kwanza alikuwa ni mwanamitindo na msanii Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye alimlipa Sh. 40,000 kwa kumfanyia ubunifu na kushona nguo maalum kwa msanii huyo.
Mbunifu wa mavazi nchini, Ally Remtullah.
Global TV Online ilifanya mahojiano na staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliyekuwa kwenyesherehe hiyo na akasema hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuhudhuria shoo iliyoandaliwa na Remtullah na alimsifia kwa kazi yake ambayo matunda yake yamekuwa yakionekana kila mahali ndani na nje ya nchi.Remtullah ni mtu mwema na anayependa kazi yake, akijaribu mambo mapya huku akiyaimarisha aliyoyapata. Kilichonivutia kwake ni kwamba mtaji alioanza nao ni mdogo sana wa shilingi elfu arobaini tu. Hivyo nawaasa Watanzania wasikate tamaa, watumie kiasi chochote cha pesa walicho nacho ili kujilete maendeleo,” alisema Lulu.
Kwa mujibu wa Remtullah, maandalizi ya sherehe hiyo yalikuwa nim akubwa na yalihudhuriwa na watu wapatao 800, wakiwemo mastaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. Idadi hiyo alisema ni kubwa akilinganisha na sherehe zilizopita ambapo zilikuwa zinajumuisha watu wapatao 500.
Remtullah aliwashukuru Watanzania kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakimpa kwa muda wote huo wa shughuli zake za ubunifu na kuwasihi waendelee kumuunga mkono kwa kumpa ushauri na maoni yoyote yanayoweza kuendeleza shughuli zake hizo.

Post a Comment

 
Top